Tukio la usalama wa mtandao wa ICRC

 

Tarehe 18 Januari 2022, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilikuwa na ufahamu wa shambulio la mtandao kwa seva zake ambapo mkosaji asiyejulikana mwenye ustadi mkubwa wa mtandao (mtu nje ya Msalaba Mwekundu) alipata ufikaji kwa hifadhidata ya Kupatanisha Uhusiano wa Familia (RFL).

Tarehe 20 Januari 2022, Msalaba Mwekundu wa Australia ilijulishwa kuhusu tukio lile.

Tutaendelea kutoa sasisho kwenye ukurasa huu kama taarifa mpya inavyopatikana.

Ikiwa unahitajika msaada wa kuongeza, au kuhitaji mkalimani, tafadhali wasiliana na simu yetu maalum ya haraka ya 24/7 kwa 1800 860 442.

Kwa wapigaji simu wa ng’ambo, tafadhali wasiliana na +61 2 8077 2507.

Kuhusu tukio la usalama wa mtandao wa ICRC

Nini ilitokea?

ICRC imegundua kwamba seva zinazofanya habari ya kibinafsi ya watu zaidi ya 500,000 ambao wanapokea huduma kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu ziliathiriwa katika shambulio la usalama wa mtandao. Msalaba Mwekundu wa Australia hutumia hifadhidata hii kwa mipango yetu ya RFL na ufuatiliaji wa kizuizi. Hatujui bado kama habari zilizoingizwa maalum na Msalaba Mwekundu wa Australia katika hifadhidata zimeathirika. Timu za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu kote duniani hutumia hifadhidata, walakini habari ambazo zinahifadhiwa katika hifadhidata zinatoka kesi yoyote tumefanya kazi nayo, kutoka nchi yoyote.

Habari ambazo umetolewa kwa Msalaba Mwekundu wa Australia ziliweza zimewekwa katika hifadhidata. Hii ni mchakato wa kawaida wa ndani kuhakikisha kuwa habari inawekwa katika eneo moja, na tunaweza kuwasiliana na wenzetu katika nchi nyingine wakati tunajaribu kutafuta mwanafamilia aliyepotezwa.

Habari hizo zinaweza kujumuisha jina lako, habari yako ya mawasiliano, habari juu ya hali za mwanafamilia wako aliyepotezwa, na majina na habari za mawasiliano za jamaa yeyote ambaye umetuambia kuhusu naye, au habari kuhusu hali ya kizuizini chako na wasiwasi uliozungumzia nasi. Zinajumuisha nyaraka zote ambazo zilitolewa kwetu katika mchakato wa kusimamia kesi yako, ambazo zinaweza kuwa pamoja na nyaraka za kitambulisho, fomu ya kuingia, vyeti vya Uthibitisho wa Kizuizini kutoka ICRC, Ujumbe wa Msalaba Mwekundu uliobadilishana kati ya wanafamilia, na picha.

Tunahakikisha kuwa kwa sasa hakuna dalili kwamba habari zako za kibinafsi zimefutwa au kuharibu nazo. Zaidi, hatujatambuliwa ushahidi wowote wa matumizi mabaya yoyote au ufichuaji wa umma wa data hii. Hii inaendelea kuangaliwa kwa karibu, na tutakujulisha ikiwa hali inabadilika.

Nini kimefanyika ili kujibu tukio hilo?

Punde tu kama ICRC ilikuwa na ufahamu wa tukio, iliondoa seva zilizoathiriwa nje ya mtandao. Hii ina maana kwamba kwa sasa hatuwezi kupata habari zozote za kesi au kazi juu ya kesi yoyote.

Sasa ICRC imo mchakato wa kutambua ufumbuzi wa muda mfupi kuwezesha timu za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu kote duniani kuendelea kutoa huduma za kibinadamu kwa watu wanaoathirika na tukio hili.

Tofauti, Msalaba Mwekundu wa Australia unafanya mapitio huru ya mifumo na huduma za eneo kuhakikisha kuwa zinabaki salama.

Pamoja, tunafanya kazi kusaidia wateja ambao wanaweza kuathirika na kuimarisha zaidi mifumo ili kuzuia tukio kama hilo kurudia tena.

Kwa nini tunakuwasliana nawe?

Tunakuwasiliana nawe kwa sababu tumefanya kazi nawe kuhusiana na moja au zaidi ya huduma zifuatazo:

 • Kutafuta na kupata jamaa aliyepotezwa kama matokeo ya vita, mkasa au uhamiaji.
 • Kutuma ujumbe kwa jamaa ambapo hakuna njia nyingine ya kuwasliana.
 • Kuangalia ustawi wa jamaa nje ya nchi ambaye hukuweza kumpata.
 • Kuomba nyaraka kuhusu mtu binafsi.
 • Kufuatilia hali za vituo vya kizuizini cha uhamiaji.

Kama matokeo ya tukio hilo, baadhi ya habari zilizotolewa kwako au kwa wanafamilia wakati wa mchakato zinaweza kuathirika. Tafadhali ongea na wanafamilia wowote ambao waliweza kuathirika na tukio hili na wanaweza kutofahamu.

Hifadhidata ya RFL ni nini?

Hifadhidata ya RFL inatumiwa na Msalaba Mwekundu wa Australia na Mashirika ya Kitaifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu kote duniani:

 • Kusaidia kutafuta watu waliopoteza.
 • Kushiriki na kuhifadhi habari kuhusu kesi za RFL, ikiwa ni pamoja na ujumbe uliobadilishana na jamaa yako katika nchi nyingine.
 • Kurikodi masuala ya wasiwasi ya kibinadamu yaliyozungumzia nasi na watu katika kizuizini cha uhamiaji.
 • Kuhifadhi mawasiliano na watu wa kizuizini cha uhamiaji.
 • Kurikodi habari kuhusu mwelekezo tumefanya kuhusiana na misaada kwa wewe na familia yako (ambayo ilijadiliwa nawe).

Hifadhidata ya RFL inafanyikwa kwa Geneva na kusimamishwa na ICRC.

Kwa nini ICRC ina habari zako za kibinafsi?

Kupatanisha Uhusiano wa Familia (RFL) ni huduma ya ulimwengu inayotolewa katika nchi kote duniani. Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, ikiwa pamoja na Msalaba Mwekundu wa Australia, hutumia mfumo wa mtandao kuhifadhi habari kuhusu kesi za RFL. Tunafanya hivi ili habari inahifadhiwa salama kwa eneo moja, na tunaweza kuwasiliana na wenzetu wa Msalaba Mwekundu katika nchi nyingine wakati wa kujaribu kupata jamaa aliyepotezwa.

Pia tunatumia mfumo huu wakati tunaposaidia watu katika kizuizini cha uhamiaji.

Ni habari gani za kibinafsi yako ambazo zimeathiriwa?

Seva za ICRC zinazofanya hifadhidata ya RFL na mifumo inayohusiana ziliathiriwa. Wadukuzi walikuwa ndani mfumo ule na walikuwa na uwezo wa kunakili na kuhamisha taarifa. Hatujui bado kama habari zilizoingizwa na Msalaba Mwekundu wa Australia katika hifadhidata ya RFL kihususa zimeathirika. Habari ambazo zinaweza zimeathiriwa ni pamoja na barua na kumbukumbu kuhusu kesi yako. Kwa ufahamu wetu, habari haijachapishwa au kuuzwa kwa wakati huu, na tunafuatilia sana hii.

Ni hatua gani za tahadhari unazoweza kufanya ili kujilinda na taarifa zako za kibinafsi?

Ambapo chama cha tatu kinaweza kupata habari yako ya mawasiliano, ni muhimu:

 • Kubadilisha nenosiri – badilisha nenosiri zako za mtandaoni ikiwa hujafanya tayari. Ikiwa ulijituma nenosiri za akaunti nyingine kwa barua pepe, badilisha hizi pia. Kituo cha Usalama wa Mtandaoni cha Australia hutoa mwongozo wa matumizi mazuri ya nenosiri.
 • Uangalifu - kama una mashaka ya anwani ya tovuti, wasiliana na mtoaji wako wa huduma kuhakikisha unaingia ukurasa sahihi. Usitoe maelezo yako ya kuingia.
 • Wezesha ulinzi wa kuongeza – anzisha uhalalishaji wa sababu nyingi kwa akaunti zako za mtandaoni inapowezekana na hakikisha una programu ya kisasa ya kupambana na virusi imewekwa kwenye kifaa chochote unachotumia ili kupata akaunti za mtandaoni.
 • Angalia viungo – kumbuka kile kinachoitwa ‘Kipatanaji cha Rasilimali ya Moja’ au ‘URL’ wakati umo kwenye ukurasa wa tovuti ambao unaomba hati zako za kuingia. Hiki kipo kwenye mstari wa anwani ya kinjari chako cha mtandaoni na huanza na ‘https://’
 • Mawasiliano ya simu ya mkononi – uwe na tahadhari kwa ajili ya huduma za simu za mkononi kuonyesha kwamba simu yako haishikamani tena na mtandao ambapo hivi siyo kawaida, au hujaielekeza huduma ya simu yako ya mkononi kukomesha muunganisho. Ambapo hii inapotokea, tunakupendekeza kujulisha huduma yako ya simu ya mkononi ya suala mara moja.
 • Angalia mwongozo wa Scamwatch – unaweza kutaka kuangalia mwongozo wa Scamwatch wa Tume ya Mashindano na Mtumiaji ya Australia juu ya kujilinda kuzuia utapeli.
 • Ili kupata mwongozo zaidi kuhusu kulinda utambulisho wako, unaweza kutaka kutembelea kwa ukurasa wa mwongozo wa Kituo cha Usalama wa Mtandaoni cha Australia.

Bado tunapitia mchakato makini wa kuelewa upeo kamili wa tukio hilo na jinsi wateja wetu wanavyoathirika. Tunaahidi kutoa kwako na sasisho zaidi kama taarifa husika inavyopatikana, ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri uliosasishwa juu ya hatua za tahadhari unazoweza kufanya.

Ikiwa ukipita dhiki, tunapendekeza kuwa upate ushauri wa afya kutoka mtaalumu wa afya aliyesajiliwa unayemjua na kumwamini.

Unaweza kupata msaada wa kuongeza wapi?

Msaada wa ziada unapatikana kwako na kwa wapendwa wako, ili kukusaidia kushughulikia na maswali yoyote au wasiwasi kuhusu taarifa hii na tukio lile. Huo ni pamoja na:

Msalaba Mwekundu wa Australia

Unaweza kupiga simu kwa simu yetu ya muhimu kwa kutumia nambari za simu zilizoorodheshwa hapa juu.

Tafadhali pia angalia tena ukurasa huu wa tovuti kwa sasisho wakati wa siku zijazo.

IDCARE

Ikiwa una wasiwasi kuhusu matumizi mabaya yanayowezekana ya habari yako ya kibinafsi, tumepanga msaada bure kutoka IDCARE, huduma ya msaada wa jamii ya utambulisho wa kitaifa na usalama wa mtandaoni ya Australia.

Tafadhali pata Meneja wa Kesi ya IDCARE kupitia Fomu ya Mtandaoni ya Pata Msaada ya IDCARE ikiwa una wasiwasi pana wa uslama wa utambulisho.

Mbadala, unaweza kutembelea Kitua cha Kujifunza cha IDCARE kupata taarifa zaidi na nyenzo juu ya kulinda habari yako ya kibinafsi. Huduma za IDCARE zinaweza kupatikana kwa kutoa msimbo wa rejea RCA-D22 wakati unapojaza Fomu ua Mtandao ya ‘Pata Msaada’ au kupiga simu kwa 1800 595 160.

Mtaalamu wako wa huduma ya afya

Ikiwa ukipita dhiki, tunakupendekeza utafute ushauri kutoka mtaalumu wa afya aliyesajiliwa unayemjua na kumwamini. Wakati unapomwona dakatari wako wa kawaidai, atatathmini msaada gani unaohitaji .

Tafadhali rejea barua pepe yetu kwa maelezo zaidi juu ya jinsi gani mashirika hayo yanaweza kusaidia kwako na wapendwa wako.

Charity donations of $2 or more to Australian Red Cross may be tax deductible in Australia. Site protected by Google Invisible reCAPTCHA. © Australian Red Cross 2024. ABN 50 169 561 394